This post is also available in: 简体中文 (Chinese (Simplified)) English (English) Français (French) Español (Spanish) Português (Portuguese, Portugal) Română (Romanian) Filipino (Filipino) Deutsch (German)
Fikiria hili: unatembea kuelekea nyumbani baada ya siku yenye kazi nyingi na unamuona mtu aliye kipofu akijaribu kuvuka barabara. Hakuna aliyemuona isipokuwa wewe. Unakimbia ili kumsaidia nakumuongoza ili aweze kuvuka salama. Unafanya kitu amabcho mtu yeyote mwenye utu angeweza kufanya.
Katika maisha, sote tuna upofu wa aina fulani. Tumetupwa kweye uwepo na hatuna muono uliowazi juu ya sababu yake. Hatujui tunaelekea wapi baada ya maisha haya. Muongozo wa Mwenyezi Mungu unatupa majibu ya maswali yalitupa upofu kutokana na kujua kwanini tupo hapa, tunatakiwa tufanye nini na tunapoelekea. Kwakuwa mwenyezi mungu ndio chanzo cha wema wote na kwamba yeye ndio mwingi wa rehma, kutoa muongozo kwa binadamu ni jinsi ya kuonyesha asili yake isiyoweza kuepukika.
Kwa njia hiyo hiyo, tunapotengeneza simu ya mkononi, gari au kompyuta, tunampa mnunuzi kipeperushi cha maelezo au maelezo ya aina nyingine.hatutaki watu wajifunze kwa kuteseka au kwa kuharibu kifaa chao kilicho ghali kwa kukitumia vibaya. Kwa kuwa mwenyezi mungu ameitengeneza dunia hii na kila kitu ndani yake, hivyo basi inaleeta maana kwamba Mweneyzi Mungu atatuambia kwanini ametuumba. Mwenyezi Mungu amuumba ulimwengu na viwango sahihi kwaajili ya sheria za kiasili zenye kustahimilisha maisha, zinazoruhusu uwepo wetu.
Pia ametupa kila kitu tulichonacho: kutoka hewa tunaipumua, matunda tunayokula, mpka familia na marafiki tulionao. Mweneyzi Mungu ametupa mahitaji yetu yote ya kimwili, kwanini basi asitupe mahitaji muhimu kwa ajili ya uwepo wetu na mahitaji ya kiroho? Kama binaadamu, tunataka kujua lengo la maisha, nini kitatokea baaada ya kifo, njia sahihi ya kuishi, kipi ni sahihi na kipi sicho- na tunataka kujua sahihi kuhusu Mweneyzi Mungu. Ni wazi kwamba Mweneyzi Mungu ndio kiini cha uwepo wetu; hivyo, inaleta maana kwamba angetaka kuwasiliana na kutuongoza.
Swali linajitokeza: wakati tuna dini nyingi na vitabu vingi vinazotofautiana, tufuate kipi? Hakika haviwezi vyote kuwa sahihi: hivyo basi labda vyote vimekosema? Ni rahisi kuyakana maandishi yote ya kidini na kusema kwamba Mweneyzi Mungu hajaturemsha chochote na kwamba dini zote zinamakosa. Hii ina ukweli kiasi: kuna dini nyingi zilizoundwa na binadamu na zinazopingana.
Ila, hakuna mantiki kusema kwamba mwenyezi Mungu hajateremsha kitu chochote kabisa: sote tuna sababu nzuri za kuamini kwamba Mwenyez Mungu atatutumia muongozo. Ingekuwa bora kuwa na mawazo pevu na kutafuta ushahidi au kujijaribu vitabu vya dini kabla hatujahukumu. Vingi vinaweza kuwa vya uongo lakini kunaweza kuwa na kimoja ambacho kinaweza kufualu mtihani.
Kitabu hichi kidogo kinalenga kuonyesha jinsi, kulingana na malengo ya vigezo vya busara, Qur’an ni neno la Mwenyezi Mungu. Hii haimaanishi kwamba Qur’an ndio ufunuo pekee uliteremshwa na Mweneyzi Mungu kwa wanaadamu. Uislamu unafundisha kwamba Mweneyzi Mungu amekuwa akiteremsha muongozo na vitabu vitukufu kwa wajumbe wake, toka kale (wakati wote toka mwanzo); Qur’an ni ufuon wake wa mwisho tu.
Upime ujumbe
Mtu yeyote mwenye akili atakubali kwamba kutathmini jinsi kitabu fulani kilichoteremshwa na Mwenyezi Mungu, itabidi kipitie kipimo fulani. Bila kuthibitisha, basi kitabu chochote kinaweza kudai kwamba kimeteremshwa na Mwenyezi Mungu. Ili kipimo hicho kichukuliwe kwa uzito, lazima kitumia vigezo vya busara vyenye maana (malengo mahususi). Hii inamanisha kwamba njia tunazotumia kuamua kama kitabu kimetoka kwa Mwenyezi Mungu au la, lazima ziweze kutumika kwenye kitabu chochote cha dini. Kipimo hicho hakiwezi kutokanana hisia binafsi, emotions, intuition na uzoefu, ila kinatakiwa kuwa kipimo kinachoweza kutumiwa na kila mtu, na kutumika kila sehemu.
Vigezo hivi vya busra lazima vizingatie:
- Dhana ya Mwenyezi Mungu lazima iwe wazi, yenye kueleweka na yenye mantiki. Haina/ haileti mantiki Mwenyezi Mungu awe ni yule asiyemkamilifu, aliye kama binadamu na haiuridhishi moyo wala akili. Ujumbe juu ya uhusiano wetu na Mweneyzi Mungu unatakiwa uwe wazi na wenye mantiki pia. Haitoleta maana kama kitabu cha Mwenyezi Mungu kitaagiza aabudiwe na anyenyekewe asiye Mwenyezi Mungu.
- Kinatkiwa kiwe na ulingano wa ndani na wa nje: ka kitabu kinasema kwenye ukurasa wa 20 kwamba kutoa sadaka ni jambo jema halafu kwenye ukurasa wa 340 kikasema kutoa sadaka ni jambo baya, basi kitabu hichi kitakuwa hakina ulingano wa ndani. Pia, kama kitabu kinasema kwamba mwezi umetenenzwa kwa jibini, basi kitakuwa hakina ulingano wa nje. Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu hakiwezi kuwa na tofauti
- Lazima kiwe na ishara kwamba kimetoka kwa Mwenyezi Mungu. Ufunuo lazima uwe na kitu kiashiriacho kwamba umetoka kwa Mwenyezi Mungu.
Tututumia vigezo hivi kwenye Quran, ili kutusaidia kuelewa kama ni ufunuo wa Mwenyezi Mungu.
- Dhana ya Mwenyezi Mungu katika Quran
Kama kuna kitabu kinasema kwamba Mwenyezi Mungu ni mtu mkubwa mwenye ndevu ndefu nyeupe aliye angani, tunaweza kukubaliana moja kwa moja kwamba kitabu hicho hakijatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni kwa sababu uwezo wetu wa kufikiri unatuwezesha kufahamu kwamba Mwenyezi Mungu lazima awe nje ya ulimwengu huu na awe mweney kujitegemea. Binadamu, hata aweje , ni kiumbe tegemezi. Hii ni kwa sababu ya sifa kama ukubwa, umbo, rangi ambazo ni sifa zenye mipaka kama. Vitu vyote vyenye sifa zenye mipaka ni vitu tegemezi kwa sababu kuna vitu vya nje vinavyosababisha mipaka yao. Mwenyezi Mungu hayupo “kimwili” na hujitegemea, kwa sababu yeye ndiye aliyeuumba ulimwengu huu. Hivyo basi, hakuna aliye na sifa za kimwili anayeweza kuwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa viumbe vyote na kimantiki hatakiwi kufanan na viumbe vyake. Mwenyezi Mungu sio kama viumbe na pia hawezi kuwa miongoni mwa viumbe.
Muono wa Quran juu ya Mwneyezi Mungu ni ya intuition ya kufikirika kibusra na inayoendana kimantiki. Aya zifuatazo ni miongoni mwa yaa zisomwazo sana kweny Quran, ambapo Allah anajitambulisha kama:
Aya hizi kutoka kweny Quran ziliteremshwa kama jbu kwa Mtume Muhammad (saw) pale alipoulizwa kuhusu uhalisia wa Mwenyezi Mungu. Ukisoma mara moja tu unapata uelewa ulio wazi juu ya kinachosemwa na utaelewa kwamba dhana ya Mwenyezi Mungu inaleta maana:
Mungu ni mmoja. Haiwezekani kuna na nguvu mbili kubwa zilizopo kwa wakati mmoja, isipokuwa mmoja atazuia nguvu za mwingine. Maana ya Mungu ni yule asiyeweza kuzuiliwa- hakuna kitu kutoka nje kinachoweza kumuwekea mipaka- kwa hiyo ni mmoja. Mungu ndiye muumba pekee anayestahili ibada na kunyeyekewa. Yeye ndiye mmoja, umoja wake hauwezi ubadilishwa kwa njia yoyote, ikimaanisha kwamba hauwezi kumgawanya vipande vipande. Ingawa dini nyingine husema kwamba Mungu ni mmoja Uislamu ni wa kipekee kwa kuwa unasema Mungu pekee ndiye anayestahili kuabudiwa. Dini nyingine zinaweza kudai kumuabudu Mungu mmoja lakini wanaweza wasimpkweshe kwenye ibada. Quran inaweka wazi kwamba Mwenyezi Mungu pekee yake ndiye anayestahili kuabudiwa na kuombwa.
Mwenyezi Mungu ni wa milele. Hajaumbwa. Angekuwa ameumbwa, angehitaji muumba. Kitu kinachohitaji muumba hakiwezi kuwa Mungu. Mungu pekee ndiye Muumba, bwana na mlezi wa kila kitu kilichopo. Hakuna kinachotokea bila ruhusa yake. Mwenyezi m\ungu pekee ndiye anayeweza kutupatia mahitaji yetu yote na hivyo ki ukweli; yeye pekee ndiye tunayemtegemea kikamilifu.