This post is also available in: 简体中文 (Chinese (Simplified)) English (English) Français (French) Español (Spanish) Português (Portuguese, Portugal) Română (Romanian) Filipino (Filipino) Deutsch (German)
Fikiria kama ungejikuta mfungwa katika nchi ya kigeni. Umefungwa humo kwa wiki kadhaa.
Siku moja, walinzi wawili wakaja gerezani kwako. Akiambatana nao ni mtu aliyevaa suti na kubeba mkoba wa kahawia. Wamesimama mbele ya mlango wa gereza lako. Mtu aliyevaa suti akatoa karatasi kutoka kwenye mkoba wake. Akalitaja jina lako kisha akakukabidhi karatasi hiyo. Inasema:
Takribani saa moja baada ya kusoma ujumbe huu, utakufa. Inaweza kuwa zaidi ya saa moja au kidogo yake, lakini muda wako ukiisha hautoweza kuikimbia adhabu, Kifo! Hakuna aliyeweza kuikimbia adhabu hii isipokuwa kwa njia moja tu. Wale waliomaliza jukumu moja rahisi. Ukilikamilisha jukumu hili utaishi. Hakika sio kuishi tu bali maisha yako yatakuwa bora zaidi kuliko unavyoweza kufikiria.
Jambo hili halitachukua hata dakika tano za saa yako moja iliyobaki. Jukumu hili ni kumpigia simu mama yako na kumwambia kwamba yeye ndiye mama pekee uliyenae, unamthamini na unashukuru kwa yote aliyowahi kukufanyia na kwamba unamuomba msamaha kwa lolote ulilowahi kufanya na likamuudhi. Ni hilo tu. Utapewa simu ya mkononi. Namba ya mama yako ipo ndani ya simu hiyo, itafute namba yake umpigie. Una saa moja ya kufanya hivyo.
Unapomaliza kusoma unatizama juu. Mtu hyo aliyevaa suti anakukabidhi simu ya mkononi na anakuacha na walinzi. Utafanya nini?
Linaonekana jambo dhahiri sana, lakini hujapewa taarifa kwamba simu hii pia ina meseji zako na akaunti za mitandao ya kijamii, na pindi unapoiwasha tu barua pepe na taarifa kutoka kwenye mitandao yako ya kijamii zinaanza kuonekana kwenye skrini, akiwemo mwanasheria wako ambaye amekuwa akikutumia ujumbe kwamba anaweza kukutoa.
Bila kufikiria unaanza kutizama meseji zako, kuzisoma na kuzijibu! Zinakupotosha mara tu ulipoanza na zinaendelea kuchukua muda wako. Kwa mbali unakumbuka kwamba una saa moja tu lakini unaendelea kujiambia kwamba una muda wa kutosha. Baada ya nusu saa mlinzi anakuja. Kisha anakuuliza, “Umekamilisha jukumu lako?”
Unamtizama huku ukishangaa, bila hata kukumbuka kwanini ulipewa simu hiyo. Mlinzi huyo anaondoka na mara simu kutoka kwa mwanasheria zinaanza kuingia. Unapokea. Anakuahidi kwamba atakutoa na kukutaarifu kuwa mradi mdogo ulioanzisha nae unatoa pesa nyingi sana.
Kila mtu anazungumzia jinsi ulivyokuwa tajiri na kwamba hakuna anayeweza kukufanya lolote maana una thamani zaidi ukiwa hai. Mara unasikia sauti za mtu akitembea, unatizama na kuwaona walinzi tena. Sita mara hii, wamevaa nguo nyeusi na kubeba minyororo mizito.
Saa imekwisha!
Huu ni mfano wa maisha yetu ya duniani. Maisha yako hata yawe marefu kiasi gani, kiuhalisia ni kama saa moja tu katika siku. Kipindi tu. Katika kipindi hichi cha maisha yako una jukumu rahisi tu. Kubali kwamba kuna Mungu mmoja tu. Kufanya hivi ni jambo la kiaisilia, lenye maana na dhahiri zaidi. Ndani ya moyo wako tayari unajua kwamba yupo aliyemkubwa, mwenye busara na mwenye nguvu kuliko wote aliyekuumba wewe na ulimwengu huu na ndiye anayekupa wewe riziki yako na kutawala vitu vyote. Kubali neema zake na uombe msamaha wake.
Mshukuru yeye na yeye peke yake. Muabudu peke yake na usimfanye mwingine yeyote kuwa sawa na yeye. Haichukui muda mwingi wa maisha yako kufanya hivyo. Maisha yako ni kama dakika tano katika ile saa moja. Ukifanya hivi utaipata furaha ya milele, pepo. Sehemu yenye amani kamili, furaha na mahali ambapo kuna kila kitu ambacho umewahi kukiota na kukitamani, na zaidi yake. Vitu ambavyo moyo wako hauwezi hata kuvifikiria, na ubongo wako hauwezi kuviwaza.
Hautozeeka katu, hautokuchoka, wala kuchoshwa, wala kuhisi njaa wala kiu, wala kuhisi joto sana wala baridi sana. Kila wakati ndani yake utakuwa bora zaidi ya wakati uliopita.
Lakini maisha haya ya dunia yanakupotosha!
Yanakupotosha mpaka wakati muda wako ukiisha, lakini ukifika hapo unakuwa umechelewa sana! Hakika ukiwa kaburini utajua kwa hakika ukweli kwamba maisha haya yalikupotosha na kwamba maisha haya yalikuwa mtihani. Kufaulu mtihani huu kulihusisha jambo jepesi sana, rahisi na la kiasilia.
Kushuhudia kwamba kuna chanzo kimoja tu cha kweli cha mafanikio; Muumba, asiyekuwa na yeyote aliyesawa nae wala mpinzani. Kumuomba Muumba wako msamaha kwa sababu ya makosa yako na kumshukuru kwa kujitahidi kuishi maisha yako kulingana na muongozo aliyoutuma.
Lakini maisha haya ya dunia yanakupotosha!
Kifo ni uhalisia utakaotukumba wote. Ni jambo la uhakika kabisa. Hauwezi kukitoroka kifo.
Matajiri kwa masikini, mwenye afya na wagonjwa, vijana na wazee, wanaumwe kwa wanaume, weusi na weupe kutoka Mashariki na Magharibi, kifo kitawafikia wote. Hivyo basi,umeandaa nini kwa ajili ya maisha yajayo? Umefanya nini kujiepusha na hatari yake na majaribu yake?
Hivi kweli unafikiria kwamba utaachwa tu na usiwajibishwe kwa yote ambayo umeyafanya au kwa yale ambayo ulishindwa kuyafanya? Hapana, hakika utaulizwa. Uzito wa chembe ya wema au ubaya, utawekwa dhahiri siku ambayo haina shaka ndani yake.
Hii ni siku ya hesabu. Siku ya malipo. Siku ya Kiyama. Udhalimu na uovu wote utasahihishwa, na utapewa daftari la matendo yako. Yeyote ambaye mzani wake utakuwa mzito kwa matendo mema ataenda kwenye bustani za furaha.
Yeyote ambaye mzani wake wa matendo ni mzito kutokana na matendo maovu, watapata moto uwakao, uliojaa maumivu yasiyoisha na mateso, ambapo watu waliondani yake hawataishi wala hawatakufa,mateso yatakayoongezeka tu milele. Kifo kitawakabili kutoka kila kona lakini hawatokufa.
“Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.
Qur’an sura ya 57 aya ya 20
Fikiria.
Unataka kuwa wapi katika maisha yako ya milele?