This post is also available in: 简体中文 (Chinese (Simplified)) English (English) Português (Portuguese, Portugal) Română (Romanian) Filipino (Filipino)
Takriban Wakristo bilioni mbili na Waislamu bilioni moja na nusu wanamuamini, ila inawezekana Yesu akawa mtu aliyetafsiriwa vibaya kuliko watu wote katika historia.
Kitabu hichi kinachunguza na kuweka uwazi juu ya Yesu, maisha yake, mafundisho yake, haiba na ujumbe wake. Kinaonyesha yanayofanana katika Ukristo na Uislamu na pia kuchambua tofauti kati ya dini hizi mbili.
Kitabu hichi kinaelezea wapi na jinsi gani Quran inatoa changamoto kwa masimulizi ya Kikristo. Kwa kufanya hivyo, inampa msomaji uelewa thabiti na uliowazi juu ya Yesu na ujumbe wake wa kweli. Kitabu hichi kinaonyesha kwanini Uislamu ni ‘kiungo kilichokosekana’ na daraja muhimu linalounganisha Uyahudi na Ukristo, hivyo kuunganisha dini zote za Kiibrahimu.
“Kitabu chenye majereo kamili na tafiti za kisasa, kilichoandikwa kwa mtindo ulio rahisi kusoma, kitabu hichi kitabadilisha muono wako juu ya Yesu na ujumbe wake milele!”
MUHTASARI WA KITABU
- Historia ya Utatu: Kuna maoni mengi juu ya Yesu katika kanisa la awali na jinsi utatu ilivyobadilika karne baada ya karne.
- Utatu dhidi ya Biblia: Kwanini utatu hauendani na biblia.
- Yesu katika Uislamu: Jinsi Uislamu unavyorejesha ujumbe halisi wa Yesu wa kumuabudu Mungu mmoja tu.
- Utume: Jinsi Uislamu unavyourekebisha muonekano wa mitume wa Mungu uliotiwa dosari katika Biblia.
- Bila damu, hakuna msamaha: Kwanini thiolojia ya msalaba inapingana na msimamo wa upendo wa Mwenyezi mungu, uadilifu na rehema yake.
- Kusulubiwa: Kwanini kifo cha Yesu msalabani ni tukio ambalo limeeleweka vibaya zaidi kuliko tukio lolote kwenye historia.
- Kuhifadhiwa: Kwanini Quran ndio maandiko pekee katika historia yaliyohifadhiwa bila dosari.
- Paulo: Mgogoro wake na wafuasi na jinsi alivyopotosha ujumbe wa Yesu.
- Ufichwaji mkubwa: Jinsi Ismail alivyofutwa kwenye Biblia.
- Utabiri: Jinsi Biblia ilivyotabiri ujio wa mtume Mwarabu baada ya Yesu.