This post is also available in: English (English) Español (Spanish) Português (Portuguese, Portugal) Română (Romanian) Filipino (Filipino)
Ili kusilimu na kuwa muislamu, mtu anahitaji kutamka maneno yafuatayo tu, kwa yakini na uelewa:
Kwa Kiarabu: “Laa ilaaha illa Allah, Muhammad rasool Allah.”
Yanayomaanisha: nashuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mjumbe (Mtume) wa Mwenyezi Mungu.”
Ni rahisi kiasi hichi.
Vitu vya kuzingatia:
[1] Quran imeteremshwa kwa lugha ya kiarabu [2] Allah ni neno la Kiarabu linalomaanisha Mwenyezi Mungu [3] Kimsingi unayakinisha moyoni mwako kwamba Mwenyezi Mungu ndiye pekee anayestahili kuabudiwa na kwamba Muhammad (na sio mwingine) ndiye aliyekuja kutufundisha jinsi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu. Ndio maana kama Waislamu, tunamheshimu Muhammad na kufuata mafundisho yake, hali ya kukubali kwamba yeye bado ni binadamu na sio mungu.Kwa undani zaidi:
Neno “Muislamu” linamaanisha mtu aliyejisalimisha kwenye mipango ya Mwenyezi Mungu, bila kujali rangi ya ngozi, taifa au asili ya kikabila. Kuwa Muislamu ni mchakato rahisi ambao hauhitaji vigezo vyovyote. Mtu anaweza kusilimu peke yake kwa faragha au anaweza kufanya hivyo mbele ya watu.
Kama mtu ana nia ya kweli ya kuwa Muislamu na ana yakini na imani thabiti kwamba Uislamu ndio dini ya ukweli ya Mwenyezi Mungu, kisha, kitu pekee anachotakiwa kufanya ni tutamka shahada, uthibitisho wa imani, bila kupoteza muda. Shahada ni nguzo ya kwanza na muhimu zaidi katika nguzo tano za Uislamu.
Kwa kutamka ushuhuda huu au shahada, kwa imani thabiti na yakini, mtu huingia katika Uislamu.
Kwa kuingia kwenye Uislamu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake, dhambi zetu zote za zamani husamehewa, mtu huanza maisha mapya ya uchamungu na uongofu. Mtume alisema kumwambia mtu aliyemuwekea sharti la kwamba Mwenyezi Mungu amsamehe dhambi zake pindi atakapokubali Uislamu:
Je, hujui kwamba kusilimu kunafuta dhambi zote kabla yake ?”
Mtume Muhammad (saw)
Mtu atakapoukubali Uislamu, kimsingi anatubu kutokana na mambo na imani ya maisha yake ya zamani. Mtu asielemewe na dhambi alizofanya kabla ya kuukubali Uislamu. Rekodi ya mtu hufutwa na huwa kama siku aliyozaliwa na mama yake. Itabidi mtu ajaribu kadri awezavyo kuiweka rekodi yake safi na kujitahidi kufanya mambo mema kadri awezavyo.
Quran tukufu na hadeeth (misemo ya Mtume) inasisitiza umuhimu wa kuufuata Uislamu. Mwenyezi Mungu anasema:
Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu…” Quran Sura ya 3 aya ya 19
Katika aya nyingine ya Quran, Mwenyezi Mungu anasema:
“Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri”. Quran sura ya 3 aya ya 85
Katika hadith, Mtume Muhammad (rehema na amani iwe juu yake), mtume wa Mwenyezi Mungu, amesema:
Yeyote atakayeshuhudia kwamba hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, asiye na mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wake na mtume wake, na kwamba Isa ni mja wa Mungu na mtume wake, na neno lake alilompelekea Mariamu na roho kutoka kwake, na kwamba pepo ni ya kweli na moto ni wa kweli, Mwenyezi Mungu atamuingiza peponi kutokana na matendo yake.” Sahih Bukhari
Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake pia amesema:
Hakika Mwenyezi Mungu ameuharamisha moto juu ya asemaye: “Nashuhudia kwamba hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ili kutafuta wajihi wa Mwenyezi Mungu.” Mtume Muhammad (saw)
Ushuhuda wa imani (shahada)
Ili kusilimu na kuwa muislamu, mtu anahitaji kutamka maneno yafuatayo tu, kwa yakini na uelewa:
Nashuhudia “Laa ilaaha illa Allah, Muhammad rasool Allah.”
Yanayomaanisha:
Nashuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mjumbe (Mtume) wa Mwenyezi Mungu.” ushuhuda wa imani
Mtu atamkapo kauli hii kwa yakini, basi atakuwa Muislamu. Unaweza kuyasema mwenyewe au bora zaidi yanaweza kusemwa na mshauri kupitia “usaidizi mubashara” hapo juu, ili tuweze kukusaidia kutamka vizuri na kukupa vyanzo muhimu kwa ajili ya Waislamu wapya.
Sehemu ya kwanza ya kauli hii inahusisha ukweli muhimu zaidi Mwenyezi Mungu aliyowadhihirishia binadamu: kwamba hapana mungu anayestahili kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu mtukufu. Mwenyezi Mungu anasema katika Quran:
Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu. -Quran sura ya 21 aya ya 25
Hii inaonyesha kwamba njia zote za ibada, iwe kuswali, kufunga, kuomba dua, kujikinga na mabaya na kutoa wanyama kama sadaka, lazima vielekezwe kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kuelekeza aina yoyote ya ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu (iwe malaika, mtume, Yesu, Muhammad, mtakatifu, sanamu, jua, mwezi, mti ) huonekana kama kupingana na ujumbe wa msingi wa Uislamu, na ni dhambi isiyosameheka isipokuwa kama mtu atatubu kabla ya kufa. Aina zote za ibada lazima zielekezwe kwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Kuabudu kunamaanisha kufanya matendo na kusema kauli zinazompendeza Mwenyezi Mungu, vitu ambavyo ameviamrisha au kuvihamasisha vifanywe, aidha kwa ushahidi wa kimaandishi au kwa kulinganisha. Hivyo ibada haiishii tu kwenye kutekeleza nguzo tano za Uislamu, lakini huhusisha vipengele vyote katika maisha. Kutafuta chakula kwa ajili ya familia na kusema kauli njema ili kumchangamsha mtu pia hukusudiwa kama ibada kama vikifanywa kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu.Hii inamaanisha kwamba ili kukubaliwa, ibada zote lazima zifanywe kwa dhati kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake.
Sehemu ya pili ya kauli hii inamaanisha kwamba Muhammad ni mjumbe aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu. Hii inamaanisha kwamba mtu atii na kufuata maamrisho ya mtume. Lazima aliyoyasema yaaminiwe, mafunzo yake yafuatwe na aliyoyakataza yaepukwe. Hivyo basi lazima mtu amuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, kutokana na mafundisho yake peke yake, kwa kuwa mafundisho yote ya Mtume yaliteremshwa kwake kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Itabidi mtu ayarekebishe maisha yake na tabia yake na kumfuata mtume, kwa sababu alikuwa mfano wa kuigwa kwa ajili ya binadamu. Mwenyezi mungu anasema:
“Na hakika wewe una tabia tukufu”. – Quran sura ya 68 aya ya 4
Mwenyezi Mungu pia amesema:
“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana”.- Quran sura ya 33 aya ya 21
Sehemu ya pili ya shahada hutekelezwa kikamilifu kwa kuufuata mfano wa mtume katika kila kipengele maishani. Mwenyezi Mungu anasema:
“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi…” Quran sura ya 3 aya ya 31
Tunakukaribisha katika Uislamu, na kukupongeza juu ya maamuzi yako. Wewe ni Muislamu sasa. Sasa, nini kinafuata? Unaelekea wapi ukitoka hapa? Tafadhali tazama programu za IERA za Waislamu wapya, zilizowekwa kwa ajili ya kuwakaribisha, kuwawezesha na kuwaelimisha Waislamu wapya.